Posts

Showing posts from September, 2021

Sababu ya mwanaume kunya kitandani alipokuwa kalala na mke wake

Image
Jamaa flani alikuwa amelala na mkewe. Mara akamuona mtu amesimama kitandani. Jamaa akafoka, “Toka hapa, we ni nani mpaka unakuja kitandani mwangu?” Yule mtu akajibu, “Mi ni malaika na hapa sio kitandani mwako uko mbinguni!” Jamaa, “Huh! Inamaana nimekufa,mbona mi bado kijana… naomba nirudishwe!” Malaika, “Inawezekana lakini siwezi kukurudisha kama mtu labda urudi kama mbwa ama kuku.” Jamaa akakumbuka mbwa wanavyopata taabu ya kulinda, akaonelea arudi kama kuku. Malaika akamgeuza kuku, akamwambia ajifunze kutaga kabla hajapelekwa duniani. Akachuchumaa na kuanza kujikamua; yai la kwanza likatoka. akajikamua tena, yai la pili likatoka. Akajikamua tena mara ya tatu. Wakati yai la tatu linatoka… akashtukia amepigwa konde ikifuatwa na sauti ya hasira ya mkewe, “Pumbav*! Balaa gani hii…. unakuny* kitandani!!”

Dunia ina mambo! Angalia kilichotokea baada ya mgonjwa kuwekewa macho ya paka

Image
  Kuna jamaa alipata ajali akapofuka macho👀, akaenda hospital akawekewa macho ya paka🐈🐱, dokta akamuuliza: vipi saizi unaona? jamaa: naona ila naona panya tu 👀🐀🐁🐀👀

Angalia alichokifanya huyu sharobaro kanisani

Image
Huu usharobaro mwingine uchizi. Jamaa kamzimia demu kanisani, mara ukafika mda wa kutoa sadaka, eti jamaa akamwambia ”dont worry bby” ntakulipia!!

Kilichotokea baada ya mzungu na mbongo kukaa siti moja, bongo wasanii wengi

Image
  Mzungu akamdharau sana Mbongo nakujiona anajua kila kitu duniani!, Akamwambia Mbongo waulizane maswali na Mbongo akishindwa anatoa sh.500 na endapo yeye atashindwa atatoa 100,000/=. Mzungu akauliza ni nchi ipi ilishindwa kwenye vita kuu ya kwanza ya Dunia? Mbongo akatoa 500 kuashiria hajui. Na yeye akamuuliza Mzungu ni kitu gani kikienda juu kina miguu minne na kikirudi chini kina miguu mitatu? Mzungu akafikiria akakosa jibu akatoa 100,000/= kuashiria hajui ila akataka kujua, akauliza ni nini hicho? Mbongo akatoa 500 kuashiria hata yeye hajui!. SHARE na marafiki kama umemkubali Mbongo kwa ujanja. Lakini unafikiri Mbongo huyu kwa akili hizi atakuwa ametokea mkoa gani!?.

Jinsi ya Kubana matumizi X-mass

Image
Badala yakupika PILAU tutapika TAMBI kwenye Xmas maana tutakua tumeokoa sh.15,000/= Vitunguu swaumu 2000, Vitunguu maji 1000, hiliki 1000, Magome 1000, Michele wa 2000, Soda 3000, Nyama 5000 . Fedha hizi zitatumika kununua mfuko wa cement ili tuanze kujaza kibubu cha ujenzi wa nyumba badala ya kupanga. Karibuni saana maji ya kunywa tumechemsha ndoo nzima.

Mtoto ni wa baba au wa mama? Angalia hoja za baba na mama kila mmoja anadai ni wake Mtoto ni wa baba au wa mama?

Image
  Mtoto ni wa baba au wa mama? Angalia hoja za baba na mama kila mmoja anadai ni wake Mtoto ni wa baba au wa mama? Mume alimpa mkewe talaka wakaenda mahakamani ili hakimu aamue nani akae na mtoto. MME: Akasimama akauliza hivi: Mheshimiwa hakimu hivi nikichukua ATM card nikaingiza kwenye mashine ikatoa pesa, sasa pesa zitakuwa ni za ATM au zakwangu? MKE: Akasimama na kusema: Mheshimiwa hakimu hivi ukimwaga mbegu ktk shamba la mtu mti ukiota utakuwa wa kwako au wa mwenye shamba?. Hebu tumsaidie hakimu aamue kesi hii…

Huyu daktari ni noma, cheki anachokisema

Image
Kuna Daktari wa Moyo alifariki wakamchongeaa jeneza lenye umbo la Moyo. Ghafla Daktari mwingine akaanza kucheka, watu wakamuuliza “kwanini unacheka unafurahia mwenzako kufariki?” Daktari yule akajibu “hapana mimi ni Daktari wa kutahiri nafikilia nikifa mtanichongea jeneza lenye umbo la ….

Misemo 10 bora ya kuchekesha itakayokuacha mdomo wazi

Image
  1. Mwanaume hata awe bahili vipi, hawezi kumpa mwanamke mimba nusu. 2. Hata uwe na magari mangapi chooni utaenda kwa miguu. 3. Kama ubinadamu kazi mbona hatupewi mishahara? 4. Ukichanganya wali na choroko unapata mseto, lakini hautibu malaria. 5. Hata njiwa nae ana makinda, lakini hawezi kuwa spika wa Bunge. 6. Hata uwe na haraka vipi kwenda Zenj, huwezi kupanda Jahazi ya Yusuph Mzee. 7. Umeme hauna kiuno lakini unaongoza kwa kukatika. 8. Hata uwe kauzu vipi, huwezi kujamba wakati unatongoza. 9. Hata uwe na imani kali vipi, huwezi  kusali  wakati unafanya  mapenzi . 10. Hata kizibo ni mfuniko lakini hauwezi kufunika sufuria.

Madogo wa sikuizi ni kiboko, cheki huyu alichokifanya akiwa darasani na mwalimu wake

Image
  Muda wa kwenda nyumbani ulikuwa umefika, mwalimu akasema: yeyote atakaye jibu swali langu lolote kwa usahìhi ataondoka asiye jibu atabaki. Dogo mmoja akatupa begi nje ya dirisha. Mwalimu akauliza nani katupa ilo begi nje? Dogo akajibu fasta mimi. Akafungua mlango akaenda kwao. neno moja kwa dogo

Namna wazazi wanavyoongea na mabinti katika umri tofauti

Image
  Miaka 13: Usipende wavulana ni wabaya. Miaka 18: Sitaki nikuone na yule mvulana tena! Miaka 23: Lini utatuletea mchumba wako? Miaka 26: Wenzio wanaolewa. Miaka 30: Tumekuambia kwamba acha kuchagua sana wanaume, hutaki kusikia! Miaka 33: Kuna  mtu  wa  Mungu  yupo kule anaombea unaweza kupata mchumba Miaka 36: At least pata mtoto mmoja. Miaka 39: We will take care of all the wedding bills…yeyote ni sawa sisi tutagharamia kila kitu mwanetu wee mlete tu . Miaka 45: hivi kweli nani alikuroga.?  changamkia fulsa umri ukifika

Madhara ya kwenda baa na mke ndo kama haya

Image
  Jamaa alienda Bar na mke wake wa   ndoa   wakakaa kwenye viti, wakati wanasubiri vinywaji akapita binti mmoja anayejiuza akamsogelea yule mke wa jamaa akamnong’oneza:- “AKULIPE KABISA KABLA HUJALALA NAYE, NI MGUMU KULIPA HUYOO!!. HALAFU HUWA HATUMII KONDOMU…” Unajua ni nini kilitokea?

Huyu mtoto kaongea point kweli, angalia anachomwambia baba yake

Image
Mtoto alimwuuliza baba yake, Mtoto: Baba unaweza kumwachia hilo gari lako house boy/girl akaliendesha? Baba: siwezi kumwachia gari langu hili aliendeshe ni ghali sana. Mtoto: je mnaweza kumwachia chumba chenu house boy/girl kikiwa wazi na mkaenda kazini? Baba: haiwezekani kamwe kuna vitu vya gharama na pia heshima haitakuwepo. Mtoto: unaweza ukampa house boy/girl ATM CARD yako na namba ya siri ukakuchulie pesa? Baba: mtoto unatafuta balaa sasa, unataka siku akiiba hii card akachukue pesa zote tuwe maskini, sithubutu. Mtoto: aahaaaaaa, kumbe hauwezi kumkabidhi chochote chenye thamani house boy/ girl, sasa kwa nini mnanikabidhi mimi kwa house boy/girl na nyie mnaenda kazini mpaka mnarudi kumbe mimi sina thamani kwenu eeeeh!

Tunaheshimiana sana na mpenzi wake

Image

Ukifa je?

Image

Mwanaume bora hupimwa hivi

Image

Hawa wakaka kuanzia 10k followers

Image

Sauti inatosha au niongeze

Image

Sawa sikatai maisha ni magumu

Image

Adui wa mpenzi wangu

Image

Ukiachana na mbu

Image

Aisome kwa sauti

Image

Tunajua nini kilichotokea

Image

Ukiachwa usiandike hivi

Image

Demu ananipenda sana

Image

Mimi mwenyewe ni member.

Image

Mimi nimempa wiki nzima

Image

Endelea na hao malay*** zako

Image

Chemsha maji

Image

Ukipewa kula kistaarabu

Image

Muulize kama anaweza beba mimba

Image

Mwanaume ambaye ananipa muda wake

Image

Bado hujazaliwa tu

Image

Muda wa kuoelewa ukifika

Image

Waname kama wanaume

Image

Mnipige

Image
 

True friends

Image

Kijora kilichopoa

Image

Hapa tumepigwa

Image

Ama nikae kimya

Image

Kama huna kota usiavae dela

Image

Taja sifa yao moja

Image

Ukitaka wanao wasifanane tabia

Image

Pumbavu kabisa

Image

Nimemwambia mpenzi wangu usiku mwema

Image

Kwenye kila ukoo

Image

Imagine

Image